Ad Code

UHAKIKI WA DIWANI YA WASAKATONGE

Uhakiki wa Diwani ya Wasakatonge


By Mwalimu Hayeshi Athuman
Diwani ya Wasakatonge ni miongoni mwa diwani zilizochapishwa mwanzoni mwa karne ya ishirini na moja zikionesha changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii yetu. Mwandishi wake ni mtunzi mahiri Mohammed S Khatibu.
MAUDHUI
Maudhui hujumuisha dhamira, ujumbe, migogoro, falsafa, mtazamo au msimamo wa mwandishi.
UMASKINI
Mwandishi ameonyesha kuwa jamii imegubikwa na wimbi la umaskini. Katika shairi la “Wasaka Tonge”, msanii anasema watu wanashindwa kupata mahitaji muhimu na ya lazima ya kila siku. Mfano wa watu hawa ni wabeba zege, yaya na wengineo. Anasema:
“jua kali na wasakatonge
Wao ni manamba mashambani,
Ni wachapakazi viwandani,
Mayaya na madobi wa nyumbani,
Ni matopasi wa majaani,
Lakini bado ni maskini”
MARADHI
Katika shairi la “Tina Isotibu” Tunaambiwa kuwa mbali na Bara la Afrika kuwa na tatizo la janga la umaskini, pia limeendelea kukumbwa na tatizo la maradhi. Msanii anasema,
“Lakini
Vidonge chungu ajabu,
Dawa zake hazitibu
Zimeizidisha tabu
Mgonjwa kumwadhibu
haipo tiba”
UONGOZI MBAYA (UDIKTETA)
Diwani hii imebainsha saratani ya udikteta unaoikabili dunia ya leo. Udikteta umeota mizizi katika dunia hii kiasi cha kuwafanya watu waishi kwa hofu. Katika shairi la madikteta msanii anasema,
“Itele “Mungu watu”
Bokasa, Idi, Mobutu.
mizinga nayo mitutu
Haitoi risasi
Hutoa maraisi
Walio madikteta
MAPENZI
Hii ni moja ya dhamira ambazo zimeonyeshwa na mwandishi kwa kina. Msanii anaonyesha kuwa mapenzi kati ya watu na mtu ni faraja amani na utulivu na ni kiungo kati ya mume na mke. Katika shairi la “Mahaba” msanii anasema,
“Kama mahaba wazimu, sihitaji nitibiwe
Bora niwe chakaramu, nipigae watu mawe
Kuwa kwangu mahamumu, wewe usi kusumbuwe
Dawa yangu si ngumu, mimi nipendwe na wewe”
Mshairi mengine ambayo yanazungumzia mapenzi ya dhati ni pamoja na “Nilikesha”
Na “Sili Nikashiba’ .
Vilevile msanii amezungumzia mapenzi ya ulaghai katika shairi la “Si Wewe”. Msanii anaonyesha ni kwa jinsi gani mapenzi ya ulaghai yanaweza kusababisha majeraha, hasira na majuto miongoni mwa wawili hao. Msanii anasema,
“Umeshapwelewa nchi kavu,
Wako werevu umekwisha,
Sasa unatweta
U taabani
Ni wewe ulo mlafi”
Si wewe?
UNAFIKI
Msanii amekemea suala la unafiki katika jamii zetu, mwandishi anaonyesha kuwa wapo waumini na viongozi wa dini ambao wamekuwa wakijigamba mbele za watu kuwa wako safi wakati matendo yao ni kinyume na waonavyosema, Katika shairi la ‘WASO DHAMBI, mwandishi anasema,
Misalaba, na majuba, na hotuba,
Nyingi toba, zenye hiba, na haiba,
Mambo yao,
Unafiki.

Chapisha Maoni

0 Maoni